Nasikia sauti nzuri kama ya malaika
Ni sauti toka mbinguni, sauti ya Mungu
Aniita mimi niende nikamtumikie
Anitume shambani mwake nikavune yote
Umeniita, nimeitika wito, nakuja kwako leo,
najongea mbele zako Bwana nipokee mimi,
niko tayari, nimeyaacha yote,
najikabidhi kwako,
unitume popote nami nitakwenda haraka
Ninaenda mimi naenda, ninaenda mwenyewe, ninaenda mbele za Bwana,
sitarudi nyuma. Ndugu zangu na marafiki, mniache niende,nikafanye kazi ya Bwana, nitakapotumwa .
Nilitazama moyo wako, moyo wako mwanangu, hata kabla hujazaliwa, nilikutambua,
nilikuteua mapema kati ya ndugu zako, uwekuhani wangu mimi, kuhani mkuu.
Shamba lake Bwana ni kubwa na
mavuno ni mengi,
wavunaji ndio wachache nitakwenda mimi,
nakuomba sana ee Bwana,
nipeleke shambani,
nikavune mavuno yote yaliyo tayari.
Uwe nami siku kwa siku, Bwana usiniache
unikinge na majaribu nilinde daima
nipeleke habari njema, ulimwenguni mwote,
watu wote wakutambue, wakugeukie.